Jinsi ya kuitendea nuru mpya!

Jinsi gani unapaswa kuitendea nuru mpya, au fundisho jipya, au kitu chochote kipya ambacho hukielewi na ni kigeni kwako? Je utainuka umejazwa chuki na kusema kitu hiki ni uongo na kinatoka kwa shetani, wakati hujakifanyia uchunguzi wa kina na kujua kama ni kweli au sio? Waadventista wengi hawajui jinsi ya kukabiriana na mafundisho mapya, fundisho likipitishwa na bodi ya kanisa wengi huamini asilimia 100% kwamba bodi imeongozwa na Roho Mtakatifu na fundisho hilo ni kweli, na wanasahau kwamba watu wachache wanaweza pia kujiingiza kwa siri na kuingiza kosa! Lakini wakati mtu mwingine anapokuja na nuru flani, Waadventista wengi hawajaandaliwa kukabiriana na nuru mpya, na hii ndiyo sababu Ellen White alitabiri kwamba hata mvua za masika zitakaponyesha wengi katika Waadventista hawatajua, watainuka kusema ni shetani, wakati hata hawajafanya uchunguzi wowote wa kina kujua kama jambo ni la kweli au sio.

Ili kuepuka hukumu hii ya kuhusisha kazi za Mungu kwa shetani, tunapaswa kuwa makini wakati tunaposikia ujumbe wowote ule. Hapo chini Ellen White anafundisha misingi kadhaa ambayo inapaswa kufuatwa ili kukabiriana na nuru mpya yoyote ile.

Msingi 1: Nuru Inaweza Kuja Wakati Wowote

a. Lazima Tujue Ya Kuwa Nuru Itafunuliwa, Na Asiwepo Mtu Wa Kujiingiza Kuipinga!

"Nuru mpya daima itafunuliwa kutoka kwenye neno la Mungu kwa yule ambaye yuko katika mahusiano hai na Jua la Haki. Hebu asiwepo mtu yeyote wa kuja kwenye hitimisho kwamba hakuna ukweli zaidi wa kufunuliwa. Mtafiti wa ukweli kwa bidii na maombi atapata mionzi ya thamani ya nuru tayari kuangazia kutoka kwenye neno la Mungu. Vito vingi bado vimesambaa ambavyo vitakusanywa pamoja kuwa umiliki wa masalio wa Mungu." —(Ellen G. White, Counsels on Sabbath School Work, p. 34, par. 1); pia Counsels to Writers and Editors, p. 35.1; Testimonies on Sabbath-School Work, p. 53.2; na Sabbath-School Worker March 1, 1892, par. 4)))

b. Nuru Haiwezi Kuja Mpaka Pawepo Na Utafiti Wa Bidii Wa Neno.

"Nuru ambayo Mungu ataituma kwa watu wake kamwe haitatokea mpaka pawepo na utafutaji wa bidii wa neno la kweli." —(Ellen G. White, Counsels on Sabbath School Work (CSW), p. 27, par. 1); pia Testimonies on Sabbath-School Work, p. 64.1)))

Msingi 2: Nuru Mpya Inapokuja, Tunapaswa Kusikiliza Kwa Makini

a. Nuru Yoyote Inapoletwa Hatupaswi Kukataa Kusikiliza.

"Wakati nuru mpya inapoletwa kanisani ni hatari kujifungia ninyi wenyewe mbali nayo. Kukataa kusikiliza kwa sababu mmechukizwa na ujumbe kwa mjumbe haitafanya jambo lenu kuwa kisingizio mbele za Mungu. Kuhukumu kile ambacho hamjasikia na hamkielewi haitainua hekima yenu katika macho ya wale ambao ni wanyoofu katika uchunguzi wao wa ukweli. Na kuwasemea kwa dharau wale ambao Mungu amewatuma na ujumbe wa kweli, ni upumbavu na wazimu. Kama vijana wetu wanatafuta kujielimisha wenyewe kuwa watenda kazi katika njia yake, wanapaswa kujifunza njia ya Bwana, na kuishi kwa kila neno litokalo katika kinywa chake. Hawapaswi kufanya akili zao kwamba ukweli wote umedhihirishwa, na kwamba Mungu Mwenyezi hana nuru zaidi kwa ajili ya watu wake. Kama wakijiingiza wao wenyewe katika imani kwamba ukweli wote umeshafunuliwa, watakuwa katika hatari ya kukataa vyombo vya thamani vya ukweli ambao utavumbuliwa kadri watu wanavyogeuza usikivu wao ili kutafuta mgodi wa utajiri wa Neno la Mungu." —(Ellen G. White, Counsels on Sabbath School Work (CSW), p. 32.1); pia Counsels to Writers and Editors, p. 51.1; na Testimonies on Sabbath-School Work, p. 60.1)

Msingi 3: Tunapswa Kumwomba Mungu Na Kuipima Nuru Hiyo Kwa Maandiko

a. Tunapaswa Kuipima Nuru Hiyo Kwa Maandiko.

"Wakati fundisho linapoletwa ambalo halipatani na akili zetu, tunapaswa kwenda kwenye Neno la Mungu, kumtafuta Bwana katika maombi, na kutokumpa adui nafasi ya kuja kwa tuhuma na chuki. Kwamwe hatupaswi kuruhusu roho kudhihirika ambayo walifikiwa makuhani na watawala dhidi ya Mkombozi wa ulimwengu. Walilalamika kwamba amewasumbua watu, na walitaka awaache wao peke yao; kwa maana alisababisha matatizo na mafarakano. Bwana hutuma nuru kwetu ili kuthibitisha ni roho ya namna gani tuliyonayo. Hatupaswi kujidanganya wenyewe." —(Ellen G. White, Gospel Workers (GW) 1915, p. 301.3); pia Councels to Writers and Editors, p. 43.1; na The Review and Herald August 27, 1889, par. 6)

b. Unatakiwa Kufanya Nini Wakati Unapoulizwa Kusikiliza Fundisho Jipya?

"Ukweli ni wa milele, na mgogoro kwa kosa utadhihirisha tu nguvu zake. Kamwe hatupaswi kukataa kuyachunguza Maandiko pamoja na wale ambao, tuna sababu ya kuamini, kutamani kujua nini ni ukweli zaidi kama tunavyofanya. Chukulia kuwa ndugu ameshikilia wazo ambalo linatofautiana na mawazo yako, na angekuja kwako akikutaka kwamba ukae naye chini na kufanya uchunguzi wa hatua hiyo katika Maandiko; Je utainuka juu, ukijazwa chuki, na kuyahukumu mawazo yake, wakati ukikataa kumpa usikivu wa unyoofu? "Njia sahihi pekee ingekuwa ni kukaa naye chini kama Wakristo na kuchunguza misimamo iliyotolewa, katika nuru ya Neno la Mungu, ambalo litafunua ukweli na kufumbua kosa. Kukejeri mawazo yake isingedhoofisha msimamo wake hata kidogo kama ulikuwa ni uongo, au kuimarisha msimamo wako kama ulikuwa ni ukweli. Kama mihimili ya imani yetu haitasimama katika kipimo cha uchunguzi, ni wakati ambao tunajua. Lazima pasiwepo na roho ya ufarisayo ikithaminiwa kati yetu. Wakati Kristo alipokuja kwa walio wake, walio wake hawakumpokea; na ni jambo la muhimu sana kwetu kwamba hatupaswi kufuata njia ileile ya kukataa nuru itokayo mbinguni." —(Ellen G. White, Counsels to Writers and Editors, p. 44, par. 1&2); pia The Signs of the Times February 6, 1893, par. 6; The Review and Herald June 18, 1889, par. 5; The Bible Echo October 15, 1892, par. 6; Testimonies to Ministers and Gospel Workers, p. 107.1-2; na Gospel Workers 1892, p. 127.1)))

c. Je Waasisi Waliitendea Vipi Nuru Mpya?

"Katika mwaka 1844, wakati chochote kilipokuja katika usikivu wetu ambacho hatukukielewa, tulipiga magoti na kumwomba Mungu atusaidie kuchukua msimamo wa haki, na ndipo tuliweza kuja katika uelewa sahihi na kuona jicho kwa jicho. Hapakuwa na mafarakano, hakuna uadui, hakuna kudhaniana-vibaya, hakuna hukumu potofu kwa ndugu zetu. Kama tungeijua roho ya mateso jinsi gani tungekuwa makini kuachana nayo!" —(Ellen G. White, Gospel Workers 1915, p. 302, par. 1), pia The Review and Herald August 27, 1889, par. 6; na Counsels to Writers and Editors, p. 43.2)

Msingi 4: Hatupaswi Kumwangalia Mtu Aliyekuja Na Nuru;ikiwa ungemwangalia Paulo kama mtesaji wa kanisa, usingeipokea nuru aliyopewa kuipeleka

a. Tunapaswa Kuingalia Nuru Yenyewe Kama Ni Ushahidi Wa Kweli, Na Si Kumwangalia Mtu.

"Haijarishi ni kupitia nani nuru imetumwa, tunapaswa kufungua mioyo yetu ili kuipokea kwa upole wa Kristo. Lakini wengi hawafanyi hivyo. Wakati hatua ya utata inapoletwa, wanajiingiza katika swali baada ya swali, bila kuikubali hatua ingawa imeendelezwa vizuri. O, tuenende kama watu wanaohitaji nuru! Mungu na atupe Roho wake Mtakatifu siku kwa siku, na kuiacha nuru ya uso wake iangaze juu yetu, ili nasi tupate kuwa wanafunzi katika shule ya Kristo." —(Ellen G. White, Gospel Workers (GW) 1915, p. 301, par. 2); pia This Day With God, p. 93.5; The Review and Herald March 25, 1890, par. 9; na 1888 Materials, p. 548.1)))

Msingi 5: Tunapaswa Kufanya Uchunguzi Wa Kina

a. Usiuhukumu Ujumbe Wa Mtu, Chunguza Kwanza Kama Mambo Ndivyo Yalivyo!

"Wakati unapoulizwa kusikiliza sababu za fundisho ambalo haulielewi, usiuhukumu ujumbe mpaka utakapoufanyia uchunguzi wa kina. na kujua kutoka katika neno la Mungu kwamba sio wa kutetewa. . ." —(Ellen G. White, Counsels on Sabbath School Work (CSW), p. 31, par. 2); pia Testimonies on Sabbath-School Work, p. 59.2)))

b. Wachungaji Na Watumishi Wote Pia Wanapaswa Kuchunguza Kwa Makini Nuru Hiyo.

"Wakati ndugu anapopata nuru mpya juu ya Maandiko, anapaswa kusema ukweli kuelezea msimamo wake, na kila mtumishi anapaswa kuyatafuta Maandiko kwa roho ya unyoofu ili kuona kama pointi zilizotolewa zinaweza kuungwa mkono na Neno lililovuviwa. 'Tena haimpasi mtumwa wa Bwana kuwa mgomvi; bali kuwa mwanana kwa watu wote, awezaye kufundisha, mvumilivu; akiwaonya kwa upole wao washindanao naye, ili kama ikiwezekana, Mungu awape kutubu na kuijua kweli;' 2 Timotheo 2:24,25." —(Ellen G. White, Christian Experience and Teachings (CET), p. 203, par. 3); pia Gospel Workers 1915, p. 303.2; Testimonies to Ministers and Gospel Workers, p. 30.3; na Pastoral Ministry, p. 30.2)))

c. Kila Mtu Badala Ya Kudharau Anapaswa Kuchunguza Nuru Aliyotumiwa.

"Nuru ya thamani itaangaza kwa neno la Mungu, na asiwepo mtu wa kuthubutu kulazimisha nini kitaletwa au nini hakitaletwa mbele ya watu katika ujumbe wa kuelimisha ambao [Mungu] atautuma, na hivyo kumzimisha Roho wa Mungu. Yoyote ile iwe nafasi yake ya mamlaka, hakuna aliye na haki ya kufungia mbali nuru kutoka kwa watu. Wakati ujumbe unapokuja kwa jina la Bwana kwa watu wake, hakuna mtu anayeweza asichunguze madai yake. Hakuna mtu anayeweza kudumu kusimama nyuma katika msimamo wa kutojali na kujiamini, na kusema, 'Najua kile ambacho ni kweli. Nimeridhika na nafasi yangu, chochote kitakachokuja. Sitasikiliza ujumbe wa mjumbe huyu; kwa maana najua kwamba haiwezi kuwa kweli.' Ni kutokana na kutafuta sababu kama hii kwamba manisa maarufu waliachwa katika giza la upendeleo, na hiyo ndiyo sababu jumbe za mbinguni hazikuwafikia." —(Ellen G. White, Counsels on Sabbath School Work, p. 28, par. 1); pia Testimonies on Sabbath-School Work, p. 65.1; na Manuscripts and Memories of Minneapolis, p. 203.6)))

d. Si Kuhukumu Ujumbe Bali Kuchunguza Kama Ni Wa Kweli Au La!

". . .kama ujumbe ukija ambao hamuuelewi, chukueni umakini ili mweze kusikiliza sababu ambazo mjumbe anaweza kuzitoa, mkilinganisha Maandiko kwa Maandiko, ili mweze kujua kama ujumbe huo unaungwa mkono kwa neno la Mungu, kama msimamo mnaoshikilia juu ya somo hauwezi kukatalika, kisha unazalisha sababu zenu zenye nguvu; kwa maana msimamo wenu hautatikiswa kwa kuja katika mawasiliano na kosa. . . .kufunga macho yenu ili msije mkaona, kufunga masikio yenu ili msije mkasikia, kuifanya migumu mioyo yenu katika kutojali na kutokuamini ili msije mkajinyenyekeza ninyi wenyewe na kukubali kwamba mmepokea nuru kwenye baadhi ya hatua za ukweli. Kujishikilia ninyi wenyewe mbali na uchunguzi wa ukweli sio njia ya kutekeleza amri ya Mwokozi ya 'Kuyachunguza Maandiko.' Je hivyo ndivyo kuchimba hadhina zilizofichika [kwa] kuyakataa matokeo ya kazi ya mtu flani [kama] lundo la takataka, na kutokufanya uchunguzi muhimu kuona kama kuna au hakuna vitu vya thamani vya ukweli katika mkusanyiko wa mawazo ambayo mnayahukumu?" —(Ellen G. White, Testimonies on Sabbath-School Work (TSS), p. 65, par. 2); pia Counsels on Sabbath School Work, p. 28.2))

Msingi 6: Hatupaswi Kufuata Mawazo Ya Viongozi;kama ungefuata mawazo ya viongozi kipindi cha Kristo, ungeangukia katika hukumu ya kuikataa nuru

a. Usifuate Mchungaji Wala Kiongozi Kipofu Yeyote, Kama Umeona Kabisa Kuwa Jambo Ni La Kweli. Pokea Ukweli, Aliokutumia Kiongozi Mkuu Wa Mbinguni!

"Wale ambao wanafuata viongozi hawa vipofu hufunga njia za nafsi zao katika kuupokea ukweli. Hawatauruhusu ukweli pamoja na vitu vya kimatendo unavyovichukua viathiri mioyo yao. Idadi kubwa wanakaza roho zao kwa chuki dhidi ya ukweli mpya, na pia dhidi ya nuru iliyo wazi sana ambayo inaonyesha matumizi sahihi ya ukweli wa zamani. . ." —(Ellen G. White, The Review and Herald March 4, 1875, par. 14); pia Redemption; or the Temptation of Christ in The Wilderness, p. 77.1; na Confrontation, p. 75.3)))

Msingi 7: Hatupaswi Kujiingiza Katika Kupinga Nuru; Mpaka Uwepo Ushahidi Wazi Kwamba Nuru Ni Ya Uongo

a. Tahadhari Kwa Wachungaji, Viongozi, Na Watu Wengine Wote Wanaojiingiza Katikati Ili Kuzuia Nuru Anayotuma Mungu!

"Kemeo la Bwana litakaa juu ya wale ambao wangeizuia njia, ili kwamba nuru dhahiri isifike kwa watu. Kazi kubwa inapaswa kufanywa, na Mungu anaona kwamba viongozi wetu wanahitaji nuru zaidi, ili waweze kuungana na wajumbe ambao anawatuma kukamilisha kazi ambayo ameiunda ifanyike. Bwana ameinua wajumbe na amewapa Roho wake, na anasema, 'Piga kelele, usiache, Paza sauti yako kama tarumbeta; Uwahubiri watu wangu kosa lao, Na nyumba ya Yakobo dhambi zao.' [Isaya 58:1]. Hebu asiwepo mtu wa kukimbilia katika hatari ya kujiingiza kati ya watu na ujumbe wa mbinguni. Ujumbe huu utaenda kwa watu; na ikiwa hakuna sauti miongoni mwa watu ya kuutoa, mawe kabisa yatapiga kelele." —(Ellen G. White, Gospel Workers (GW) 1915, P. 304, par. 2))

Msingi 8: Hatari Ya Kukataa Nuru

a. Je Kuna Hatari Gani Kama Ukiikataa Nuru?

"Wakati Bwana anapotuma ujumbe kwa mwanamume yeyote au mwanamke, na wanakataa kusahihishwa, wanakataa kuupokea, huo si mwisho wa ujumbe kwa jinsi yoyote. Shughuri zote zimewekwa katika kumbukumbu, na wale ambao walijishirikisha katika jambo hilo, kwa kukataa kusahihishwa, wanatangaza hukumu zao juu yao wenyewe." —(Ellen G. White, Special Testimonies Series B07 (SpTB07), p. 59, par. 1); pia Manuscript 111, December 4, 1905, par. 6; Letter 326, December 4, 1905, par. 5; na The New York Indicator February 7, 1906 par. 6))

b. Wanaokataa Nuru Ni Heri Wasingezaliwa!

"Wakati Mungu anapotuma ujumbe kwa mtu yeyote, mtumishi au daktari, kama watu wanaingiza sababu ambayo itaharibu ushawishi wa ujumbe ambao Mungu ameunda kwamba ungefanya mabadiliko katika kanuni za mtu anayesahihishwa, na kugeuza moyo wake ili atubu, ingekuwa heri kama watu hawa wasingelizaliwa." —(Ellen G. White, Special Testimonies Series B07 (SpTB07), p. 59, par. 2); pia The New York Indicator February 7, 1906, par. 7; Letter 326, 1905, par. 6; na Manuscript 111, 1905, par. 7)))

Msingi 9: Hatupaswi Kung'ang'ania Mawazo Ya Zamani;lazima tukubali kutakaswa katika kweli na kubadilisha msimamo wetu kuielekea kweli

a. Wale Ambao Hawatageuza Nia Zao Ili Kupokea Ukweli Mpya, Watakatishwa Tamaa!

"Tuna mambo mengi ya kujifunza na mengi, mengi ya kutojifunza. Mungu na mbingu peke yao ndio hawawezi kukosea. Wale ambao wanadhani kwamba kamwe hawataacha mtazamo bora kabisa, ambao kamwe hawana sababu ya kubadilisha wazo, watakatishwa tamaa. Muda mrefu kadri tunavyoshikilia mawazo yetu wenyewe na maoni pamoja na ung'ang'anizi wa kuamua, hatuwezi kuwa na umoja ambao Kristo aliomba." —(Ellen G. White, The Review and Herald (RH) July 26, 1892, par. 7); pia 1888 Materials, p. 991.7; Testimonies to Ministers and Gospel Workers, p. 30.2; Selected Messages Book 1, p. 37.3; Counsels to Writers and Editors, p. 37.1; Christian Experience and Teachings, p. 203.2)))

b. Wale Ambao Hawatachukua Hatua Nuru Inapoletwa, Wataenenda Gizani.

“Wale ambao hawatachukua hatua Bwana anapowaita, lakini wanasubiri kwa ajili ya ushahidi wa hakika na furusa za upendeleo zaidi, wataenenda katika giza, kwa maana nuru itaondolewa. Ushahidi uliotolewa siku moja, kama ukikataliwa, unaweza usirudiwe tena kamwe.” —(Ellen G. White, Testimonies for the Church vol. 3 (3T), p. 258 par. 3)

c. Kama Ushahidi Ni Wa Kutosha Tunapaswa Kuamini Nuru Hiyo, Na Si Kusubiria Ujuzi Kamilifu.

"Neno la Bwana, lililotamkwa kupitia watumishi Wake, linapokelewa na wengi kwa maswali na hofu. Na wengi watachelewesha utiifu wao kwa onyo na kemeo lililotolewa, na kusubiri mpaka kila kivuli cha kutokuwa na uhakika kimetolewa katika mawazo yao. Kutokuamini ambako kunahitaji ufahamu kamili hakutawahi kukubali ushahidi ambao Mungu yuko radhi kuutoa. Mungu Anahitaji kwa watu wake imani ambayo hutegemea uzito wa ushahidi, sio kutegemea ufahamu kamilifu. Wale wafuasi wa Kristo ambao wanaikubali nuru ambayo Mungu huwapelekea wanapaswa kutii sauti ya Mungu akizungumza nao wakati kuna sauti nyingine nyingi zinazolia dhidi yake. Inahitaji ujuzi wa kutofautisha sauti ya Mungu." —(Ellen G. White, Testimonies for the Church vol. 3 (3T), p. 258 par. 2); pia Mind, Character, and Personality, vol. 2, p. 535.2))


This website was built using N.nu - try it yourself for free.    (Click here to renew the premium)