Utabiri wa kujitenga na Imani

Nukuu zifuatazo kutoka kwa Ellen G. White, zinaongelea kuhusu swala la kujitenga kutoka kwenye imani miongoni mwetu sisi wenyewe, na kujitenga kutoka kwenye imani zilizoimalishwa na kutiwa muhuri na Roho, imani mwaka 1844-1900. Sasa ni wazi kwamba upitishwaji wa fundisho la utatu mwaka 1981 kati yetu, ilikuwa ni kujitenga na imani kwa maana imani za kiadventista ziliamini Yesu kuwa ni mtu tofauti na Baba, na ni Mwana halisi wa Mungu kwa njia ya kuzaliwa. Sitasema mengi, soma mwenyewe ujionee. Kumbuka nukuu zitaongezeka kadri utafiti unavyofanyika.

“Tunajua kitu kilicho mbele yetu. Tunajua kwamba majaribu yanatungojea. Tunajua kwamba Waadventista Wasabato ambao hawajawekwa wakfu, ambao wana maarifa ya kweli, lakini ambao wamejiunganisha wao wenyewe na mambo ya kidunia watajitenga kabisa kutoka kwenye imani, na kufuata roho zidanganyazo. Adui kwa furaha ataweka vishawishi kwao, kuwaongoza kufanya vita dhidi ya watu wa Mungu. Lakini wale ambao ni wa kweli na waaminifu watakuwa na ulinzi imara na wenye nguvu katika Mungu.” —(Ellen G. White, Letter 127, 1 July 1903, par. 15); pia Manuscript Releases, vol. 7 [Nos. 419-525], p. 186.2))

Kujitenga na imani ndicho kitu ambacho Ellen G. White alitarajia kutokea kati ya Waadventista.

"Mtume Paulo anatuonya kwamba, 'Wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.' Hivi ndivyo tunaweza kutarajia. Majaribu yetu makubwa yatakuja kwa sababu ya kundi ambalo hapo mwanzo waliutetea ukweli, lakini ambao wamerudi nyuma kutoka kwenye ukweli kuielekea dunia, na kuukanyaga ukweli chini ya miguu yao kwa chuki na kejeri." —(Ellen G. White, Review and Herald September 15, 1910, par. 3); pia The Review and Herald January 10, 1888 par. 3; na Evangelism, p. 624.5))

Baadhi huamini uongo kwamba kujitenga na imani inamaanisha pale baadhi ya watu wanapotoka nje ya dhehebu la Kiadventista ndio wanakuwa wamejitenga na imani, lakini hii ni hukumu ya kimwili na sio ukweli. Ellen White anafafanua kuwa, ni kuingiza mafundisho mapya kati yetu ambayo siyo ya kibiblia pia yanapingana na imani ya zamani.

"Makosa yataingia na mafundisho mageni yataletwa. Wengi watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani." —(Ellen G. White, Letter 79, February 17, 1905, par. 8); pia Evangelism, p. 595.1))

Ni wazi hapa, kujitenga na imani ni kuingiza mafundisho mageni, na ya kosa ndani ya kanisa, na sio mtu flani kutoka ndani ya dhehebu. Kama tuna macho ya kuona, ni kwamba tunaweza kujitenga na imani wakati bado tuko ndani ya dhehebu lilelile. Kujitenga na imani ni kuiacha kweli na kufuata uongo.

“Msidanganywe; wengi watajitenga na imani, na kuziandamia roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Sasa tunaye alpha mbele yetu wa hatari hii. Omega atakuwa wa namna ya kushitusha zaidi.” —(Ellen G. White, Sellected Messages Book 1, p. 197, par. 1904); pia Letter 263, July 24, 1904, par. 15; Manuscript Releases, vol. 7, p. 188.2; Special Testimonies Series B02, p. 16.2))

Alfa lilikuwa ni fundisho la uongo kuhusu nafsi ya Mungu lililojitokeza miaka ya 1900 na Ellen White akalikemea, na Omega aliyetabiriwa kwamba atafuata lazima liwe fundisho la uongo kuhusu nafsi ya Mungu.

"Baadhi watachukua nadharia ambazo zitatafsiri vibaya Neno la Mungu, na kudhoofisha msingi wa kweli ambao umekwisha kuimarishwa, hatua kwa hatua, na kutiwa muhuri kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Ukweli wa zamani unapaswa kuhuishwa ili kwamba nadharia za uongo ambazo zimekuwa zikiletwa na adui kwa busara ziweze kuzuiliwa. Hapawezi kuwa na umoja kati ya ukweli na kosa. Wale ambao wameongozwa katika udanganyifu tunaweza kuungana nao ikiwa tu wameachana na udanganyifu huo." —(Ellen G. White, Letter 121, March 15, 1905, par. 10); pia The Upward Look, p. 88.2))

"Kama watumishi wetu na waalimu wakijitoa wenyewe kujifunza nadharia hizi za makosa, wengine watajitenga na imani na kuziandamia roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani. Siyo kazi ya watumishi wa Injili kutoa sauti ya nadharia za shetani." —(Ellen G. White, Letter 175, May 21, 1904, par. 7); pia Mind, Character, and Personality, vol. 2, p. 718.3; na Evangelism, p. 624.3))

"Hebu kweli ambazo ni msingi wa imani yetu na zitunzwe mbele ya watu. Baadhi watajitenga na imani, na kuziandamia roho zidanganyazo na mafundisho ya mashetani. Wanazungumzia sayansi, na adui huja katikati na kuwapa wingi wa sayansi; lakini sio sayansi ya wokovu, ya unyenyekevu, ya kuwekwa wakfu, au kutakaswa na Roho. Tunapaswa sasa kuielewa mihimili ya imani yetu jinsi ilivyo,—kweli ambazo zimetufanya sisi kama watu kuwa jinsi kama tulivyo, zikituongoza juu ya hatua kwa hatua." —(Ellen G. White, Review and Herald May 25, 1905, par. 23); pia Counsels to Writers and Editors, p. 29.1))

ZITAKUJA ZAIDI.

This website was built using N.nu - try it yourself for free.    (Click here to renew the premium)