SABATO |
Jumapili ni Sabato? |
Bado unatunza Jumapili? |
Mitume na Sabato? 1 |
Mitume na Sabato? 2 |
Sabato ilibadilishwa? |
Muulize Yesu kuhusu Sabato |
Kalenda ya siku za wiki |
KUHUSU UUNGU |
Mungu mmoja ni nani? |
Yesu Kristo ni Mungu? |
Yesu ni malaika Mikaeli? |
Yesu alizaliwa na Mungu? |
Tuamini Uungu au Utatu? |
FUNDISHO LA UTATU |
Utatu ni kweli au uongo? |
Mungu ni fumbo? |
Utatu ni upagani? |
Yesu ni Mungu Baba? |
Wanateolojia na Utatu |
Utatu ni upinga-Kristo? |
MAFUNDISHO YA RCC |
Maelezo kuhusu Papa |
Ekaristi ni makufuru? |
MAONYO |
Pasaka ni upagani? |
Krismasi ni upagani? |
Mwaka mpya upagani? |
Usishiriki katika dhambi |
MENGINEYO |
Kwa ajili ya wa SDA tu |
Mafundisho ya EGW |
Kuhusu SLM |
Jisajili SLM |
2Wakorintho 4:6 “Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.”
Zaburi 119:130 “Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga.”
2Petro 1:19 “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.”
Najua wengi ambao "hawaipendi kweli" katika mioyo yao wenyewe, watanichukia kwa sababu ninawakilisha kile ambacho ni kinyume nao. Kwa hakika, nimekutana na baadhi ya watu mtandaoni ambao wameniambia "acha kufuatilia kanisa Katoliki, jifundishe wewe mwenyewe achana na kanisa letu".
Ndugu wengi kati ya dada na kaka wameongozwa kuamini mafundisho ya Katoliki yasiyo na msingi katika Maandiko; kama vile "Utatu", "ibaada ya Jumapili" n.k. Sababu kuu nashiriki ukweli kwenye tovuti/blog hii, si yoyote ile isipokuwa kama Yakobo anavyoweka wazi kwamba, "Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza; 20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi." (Yakobo 5:19-20)
Na labda baadhi ya roho zinaweza kuiona hali yao halisi na kuepuka uongo wa kanisa Katoliki na mabinti zake. "Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;" (Waefeso 5:11)
Je una swali?, Maoni?, Ushauri?, au umeona kosa lolote kwenye tovuti hii na ungependa kunijulisha? Nitumie email, au tumia ukrasa wa facebook.