Papa Francis asema, haoni tatizo kwa wachungaji na makasisi ambao ni mashoga!

"Papa Francis amezungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza katika mkutano, na kunukuliwa akizungumzia kuhusu watumishi mashoga. . . .Papa Francis amesema kuwa hana shida na mtu ambaye ni shoga na anamtumikia Mungu kikamilifu. . . .amesema, "Kama mtu ni shoga na anamtafuta Bwana na ana nia njema, mimi ni nani hata nihukumu?. . .Hatupaswi kutenga watu kutokana na hili suala. Inabidi wakubalike na kuchukuliwa ndani ya jamii". . . Chama kikubwa cha kupigania haki za mashoga nchini Marekani. . . wameonekana kufurahishwa na kauli ya Papa, na kusema kuwa, “kwa miaka kadhaa sasa tumeona mashoga na wasagaji wanaotokea Vatican wakikandamizwa,kauli ya Papa inaleta matumaini angalau.” —(Gospel Kitaa, Monday, 29 July 2013)

Taarifa hii ni ya kweli kabisa; maana haikuandikwa na Gospel Kitaa pekee, lakini pia gazeti la Raia Mwema, Aug 21, 2013 linasema Papa alizungumza maneno hayo huko Brazil, lakini hakuwa na nia ya kuleta msimamo mpya kuhusu msimamo wa kanisa Katoliki na mashoga. Lakini huu ni uongo mkubwa, kama ukisoma makala yote ya Raia Mwema, Aug 21, 2013 utaona kuwa makala hiyo inamtetea Papa kwamba hakufanya kosa kutamka maneno hayo; kwani Paulo wakati anakemea dhambi ya ushoga katika Warumi 1: 26-27 hakutofautisha ushoga kama dhambi kubwa kuliko zingine, tena makala hii wakati inaonekana kumtetea papa kwamba hakuleta msimamo mpya, lakini bado inatetea ushoga zaidi na kudai kwamba ushoga sio dhambi kubwa kuliko dhambi zingine.

Pia makala ya BBC 15 Oktoba 2014 ikizungumzia mkutano wa maaskofu 200; ambapo papa Francis aliwateka maaskofu wote kutetea ushoga mwaka 2014, BBC wanaandika: "Nguvu kubwa ya vikundi vya kutetea haki za watu wenye mapenzi ya jinsia moja ni juu ya kauli ya papa Francia aliyoitoa mwishoni mwa mwaka wa jana [2013] alipokuwa kwenye kambi ya vijana wa kanisa hilo huko Rio de Jeneiro alitoa kauli kua kama mtu anamtafuta Mungu na ana nia njema ,yeye ni nani wa kuhoji?".

Papa Francis amewahi kuzungumza maneno mengi katika mikutana na katika mahojiano na waandishi wa habari yanayotetea ushoga, BBC katika makala hiyohiyo hata wanasema kwamba: "Papa Francis anaingia katika historia ya kanisa katoliki ulimwenguni kutumia jina. . . WASENGE hadharani kuliko kutumia neno wapenzi wa jinsia moja." , Ushahidi unatosha, lakini ngoja tuongeze ushahidi zaidi kwamba papa ni kweli aliyatamka maneno hayo siku hiyo anatoka Brazil. Gazeti la Mtanzania Mon, Oct 20, 2014 linasema; "Mwaka jana [2013], Papa Francis aliwafurahisha wanaharakati za ushoga wakati alipoonekana kulegeza msimamo wake." Katika habari kama hii hii jarida la Mpekuzi Huru, Man. Oct 20, 2014 pia linashuhudia vilevile kama la Mtanzania.

Kwa ushahidi mwingi kama huu, tunathibitisha taarifa ni ya kweli, na papa kweli anaunga mkono maswala ya ndoa za njinsia moja, uamuzi unabaki kwako, kama utaendelea kudanganywa na kupotoshwa na kiongozi huyu, au utaamuka na kuchukua hatua. Ukweli ni kwamba, kama ilivyoripotiwa na BBC mwaka 2014 kwamba, wakatoliki wengi wanaliacha kanisa kwa sababu ya uovu huu wa viongozi wake kuunga mkono ushoga, talaka, utoaji wa mbimba, na matumizi ya madawa ya uzazi wa mpango.

19 Oct 2017

This website was built using N.nu - try it yourself for free.    (Click here to renew the premium)