Uhusiano wa SDA na Jukwaa la Wakristo Tanzania


Hii haipaswi kudhaniwa kama ni kushambulia Uadiventista au kanisa la Waadventista kwa ujumla, lengo kuu ni kuonyesha nini kinaendelea miongoni mwa Waadventista Wasabato, na si vinginevyo. Mungu pekee na ahukumu kwa haki."Hakuna maridhiano yoyote yapasayo kufanywa pamoja na wale waabuduo sabato ya uongo, yaani jumapili. . . Niliambiwa kuwa wanadamu watatumia mbinu zote ziwezekanazo ili kuondoa tofauti iliyopo kati ya imani ya Waadventista Wasabato na wale waabuduo Jumapili. Na katika vita hivyo ulimwengu wote utahusika, na mda siyo mrefu. Lakini huu siyo wakati wa kushusha bendera yetu. [2SM 385.1] Chini ya jina la Waadventista wa Sabato, nilionyeshwa kundi ambalo litaamuru kwamba ishara zinazotutenganisha na kututambulisha zisizingatiwe sana, kwa sababu, wao wanasema, tukizishikilia sana, taasisi zetu hazitafanikiwa. Lakini hiyo alama inayotutenganisha inapaswa kutenganisha ulimwengu wote hata mwisho wa kipindi cha rehema.” —(Ellen G. White, Selected Messages Book 2 [2SM], p. 385.1,2); pia Manuscript Releases, vol. 13, p. 69.1,2; na Manuscript 15, 1896, par. 27,28))

Kama una mapendekezo au maoni yoyote kuhusu swala hili; ambayo unaona ni vema kuyashiriki nami tumia fomu hii kuyatuma
Jukwaa la Wakristo lakabidhi amani ya nchi mikononi mwa raisi Kikwete. “Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) limetoa tamko kali kuhusu mchakato wa Katiba, na likiweka bayana kwamba ni Rais Kikwete pekee ambaye anaweza kukwamua suala hilo. Jukwaa hilo linajumuisha taasisi kubwa za madhehebu ya Kikristo ambazo ni Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (CPCT) na Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA.) [Jukwaa hilo limesema,] “Tunakuomba Mheshimiwa Rais kwamba amani ya nchi yetu sasa imo mikononi mwako hasa katika kipindi hiki cha kuandikwa kwa Katiba Mpya,” —(Mwananchi, Saturday, August 30, 2014)


"JUKWAA la Wakristo Tanzania (TCF). . .ni jukwaa linalojumuisha Taasisi kuu za Umoja wa Makanisa nchini, ambazo ni pamoja na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Jumuiya ya Makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) na Kanisa la Waadventiste Wasabato (SDA)." —(Raia Mwema, Dec 27, 2012)

"ASKOFU amesema maoni yaliyotolewa na Jukwaa la Wakristo Tanzania (TCF) juu ya Bunge Maalumu la Katiba, hayajatekelezwa na hivyo watapita kwa Watanzania na waumini wao kuwaeleza nini cha kufanya. . . alisema. . . Jukwaa hilo linaundwa na Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC), Baraza la Makanisa ya Kipentekoste (CPCT), Jumuiya ya Kikristo (CCT) na Makanisa ya Kisabato (SDA)." —(TANZANIA CLASSIC, February 23, 2017, saa 20:05:56)

This website was built using N.nu - try it yourself for free.    (Click here to renew the premium)